Vol. 9 No. 2 (2000): Nordic Journal of African Studies
Back Issues

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini

E. S. Mohochi
University of Egerton
Nordic Journal of African Studies

Published 2000-09-30

How to Cite

Mohochi, E. S. (2000). Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini. Nordic Journal of African Studies, 9(2), 11. https://doi.org/10.53228/njas.v9i2.620

Abstract

Tukichunguza hazina ya uhakiki uliofanywa katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili na kuiweka katika mizani, upande mmoja ubebe tahakiki zilizozingatia maudhui na mwingine zile zilizoangaza fani, upande wa maudhui utalemewa na uzito na kuanguka. Ni kweli kuwa umuhimu wa fasihi katika jamii unatokana na jinsi ambavyo inaimulika jamii na kuichora kwa madhumuni ya kuihakiki na kuirekebisha kutokana na udhati na uzito wa mafunzo mwafaka inayoyabeba. Ni kweli vile vile kuwa fasihi ni sanaa kutokana na matumizi ya pekee ya lugha na vipengele vingine vya fani ambavyo kwa pamoja huipa sura maalum na kuyafanya maudhui yake yatufikie katika hali na umbo linalovutia. Hali hii ndiyo huiwezesha fasihi kutuingia, ikatuchoma na kutufikirisha zaidi. Ndio nguzo ya utamu wa fasihi. Katika misingi hiyo, uendelezaji wa fasihi; hasa kwa upande wa uhakiki unapaswa kuzingatia pande zote mbili za sarafu; yaani maudhui na fani inayoyabeba maudhui hayo. Makala hii imelengwa kutoa mchango huo kwa kuupa uzito upande wa fani ya fasihi kwa kuzingatia kipengele cha usimulizi. Nao uteuzi wa usimulizi umechochewa na ukweli kuwa mbinu hii haijachunguzwa na wahakiki wengi katika fasihi ya Kiswahili. Awali ya kuchambua jinsi ambavyo mbinu hii ya usimulizi imejitokeza katika riwaya ya Nyongo Mkalia Ini, dhana ya usimulizi itafafanuliwa na nafasi yake katika fasihi kuwekwa bayana.