Vol. 11 No. 2 (2002): Nordic Journal of African Studies
Back Issues

Tathmini ya Kamusi Tano za Kiswahili

Arvi Hurskainen
University of Helsinki, Finland
Nordic Journal of African Studies

Published 2002-06-30

Keywords

  • leksikografia,
  • Kiswahili,
  • mbinu za kikompyuta

How to Cite

Hurskainen, A. (2002). Tathmini ya Kamusi Tano za Kiswahili. Nordic Journal of African Studies, 11(2), 18. https://doi.org/10.53228/njas.v11i2.361

Abstract

Makala hii inaeleza mbinu za kikompyuta za kutathmini kamusi, na inatoa pia matokeo ya tathmini ya kamusi tano za Kiswahili. Kamusi hizo ni: Kamusi ya Kiswahili Sanifu (TUKI), Kamusi ya Maana na Matumizi (OUP), Modern Swahili - Modern English Dictionary (MS-tryck), Kamusi ya Kiswahili - Kiingereza (TUKI), na Swahili - Suomi - Swahili -sanakirja (SKS). SALAMA (Swahili Language Manager), ambayo ilitumiwa katika tathimini hii, huweza kuainisha maneno ya Kiswahili na kuteua lemma za maneno katika matini. Ufanisi wa kila kamusi ulitathminiwa kwa kutumia aina tatu za matini, na matokeo yametolewa kwa njia ya matarakimu na jedwali. Tathmini inaonyesha uzuri na upungufu wa kila kamusi na kuleta mwongozo juu ya kurekebisha kamusi hizo.