Published 2003-12-31
Keywords
- Kushuka Hadhi Lugha za Jamii
How to Cite
Abstract
Lugha za jamii hapa nchini kama zilivyo lugha nyingine barani Afrika zinakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka lugha zilizoendelea ambazo hutumika rasmi kitaifa na kimataifa. Kabla ya Tanganyika (sasa Tanzania) kupata uhuru wake (1961), lugha za jamii zilikuwa na hadhi ya juu kijamii kuliko ilivyo sasa. Hii ilitokana na lugha hizo kutumika katika utawala wa ngazi za chini. Huku kushuka hadhi kwa lugha za jamii kumetokana na mabadiliko ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Mabadiliko haya yalisisitiza umuhimu wa sera ya lugha kukuza na kuendeleza lugha moja muhimu ili kujenga umoja wa kitaifa. Ili kuinua hadhi ya lugha za jamii hapa nchini, makala haya yanapendekeza zitumike mbinu mbalimbali zifuatazo: Kwanza, wazungumzaji wa lugha hizi wahimizwe kutumia lugha zao za jamii mara kwa mara. Pili, sera ya lugha ya Tanzania ifanyiwe marekebisho ili itoe nafasi kwa lugha za jamii kutumika rasmi. Tatu, vyombo vya habari navyo vihimizwe kutumia lugha za jamii katika mawasiliano yake na nne, lugha za jamii zipewe haki ya kutumika kisheria hapa nchini.